HERI YA MWAKA MPYA

HERI ya mwaka mpya wadau wangu wote, ni jambo la kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kuuona mwaka mpya wa 2011 kwani kuna wengine walibakiza saa, dakika ama sekunde kadhaa wakaiaga dunia bila kuuona.
Nawashukuru wadau wote/bloggers wenzangu kwa ushirikiano pia kuwa karibu nami kwa mwaka uliopita, hibvyo naomba kasi hiyo iendelee na kwa mwaka huu.
Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi wote ambao nimewakwaza kwa namna moja ama nyingine kupitia kazi zangu,pia kuwasamehe wale wote walionitendea mabaya.
Nawatakia afya njema, kila la heri katika ujenzi wa taifa.

Comments