DOGO JANJA ASEMA YEYE NI MUZIKI NA SHULE

MAMAPIPIRO NA DOGO JANJA
MSANII mdogo kuliko wote wanaotamba kwa sasa hapa nchini Abduaziz Chende maarufu kama Dogo Janja amesema pamoja na umaarufu alioanza kuupata kamwe hawezi kulipa kisogo suala la elimu.

Mwanahip hop huyo mwenye miaka 14 amesema kuwa anaamini eklimu ndiyo ufunguo wa maisha hivyo kutokana na umri wake kuwa mdogo hawezi kupoteza haki yake hiyo ya msingi sababu ya muziki.

Kwa sasa msanii huyo aliyekuwa akiishi jijini Arusha yupo jijini Dar es Salaam na tayari ameshaanza kidato cha kwanza katika sekondari ya Makongo, huku akiendelea na muziki.

Yatari msanii huyo ambaye anafanya kazi chini ya kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese, Dar es Salaam amekamilisha yake ya pili iitayo I Get Money akimshirikisha Godzillah.

Awali alitoka na Anajua aliowashirikisha Madee na Tundaman

Comments

  1. Alilosema ndilo sahihi. Tatizo ni kuwa wengi husema hivyo kwa kuwa wamekariri hivyo, na kisha hutenda visivyo.
    La muhimu si kusema kama hatotenda. Na naamini kwa kusema huku, ameweka AHADI ndani mwake na kwa wale wamsikiao ili asiweze kuivunja
    DOGO JANJA....Ujanja umeuona kuwa ni zaidi ya jina. Ni uwezo wa kuelewa na kupambanua mambo (hata mikataba ya kazi) na sehemu rahisi kuwezesha hilo ni SHULENI
    KILA LA KHERI KATIKA KUSAKA UJANJA HALISI
    Blessings

    ReplyDelete

Post a Comment