AFANDE SELE AJIKITA KATIKA FILAMU MWAKA 2011


AFANDE SELE
MSANII mahiri katika medani ya muziki wa kizazi kipya nchini, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ wa Morogoro, amesema mkakati wake mwaka 2011 ni kujikita zaidi katika filamu na mambo ya kijamii.
Afande Sele alisema, kwa kuanza anakamilisha kazi ya filamu iitwayo ‘Haki iko Wapi’, ambayo itaingia sokoni hivi karibuni.
Alisema kuwa, anaamini filamu atakazozitoa zitakuwa zenye kuvutia na kuelimisha kwa kiasi kikubwa, zikielezea maisha halisi ya wasanii wa hapa nchini pamoja na jamii kwa ujumla.
Katika filamu zake atatumia nyimbo zake za zamani na za sasa hivi na kwamba, hatatengeneza filamu zisizo na maadili mema na mila za Kitanzania, bali zote zitakuwa zenye kuelimisha.

Comments