YANGA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA ATLETICO PARANAENCE YA BRAZIL


TIMU ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam Januari 9 inatarajia kucheza mchezo mmoja wa Kimataifa na timu ya Atletico Paranaense ya Brazil kwa ajili ya kujiweka sawa na mashindano ya kuwania kombe la Shirikisho.
Ofisa Habari, wa Yanga, Louis Sendeu alisema awali kabla ya mchezo huo, kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic aliwasilisha ombi la michezo tisa ya kirafiki kwa ajili ya mashindandano ya kuwania kombe la Shirikisho.
Kabla ya mechi hiyo, Yanga itacheza na FC Leopards Desemba 26 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Comments