WAREMBO MISS TZ NA SHUGHULI ZA KIJAMII MIKOA YA KASKAZINI NA ARUSHA




PRESS RELEASE
14 December 2010


WAREMBO MISS TANZANIA KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA JAMII MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO.

Baadhi ya warembo wa Miss Tanzania 2010 wakiongozwa na Miss Tanzania 2010 Genevieve E. Mpangala watakuwa na ziara ya shughuli za jamii katika mikoa ya Kaskazini, Arusha na Kilimanjaro kuanzia tarehe15 hadi 20 Desemba 2010

Katika ziara hiyo warembo hao watatembelea baadhi ya vituo vya kulelea watoto yatima, Ikiwa ni pamoja na kuwatembelea baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wanaosoma na kuishi katika mazingira magumu.

Ziara hii imedhaminiwa na Ndege Insurance, pamoja na Vodacom Tanzania Limited

Warembo watakaohusika katika ziara hiyo ni kama ifuatavyo:-

1) Genevieve Emmanuel
2) Glory Mwanga
3) Anna Daudi
4) Buduri Ibrahim
5) Christina Justine
6) Prinsca Mkonyi
7) Furaha David
8) Salma Mwakalukwa.

HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI.

Comments