WANAMITINDO GIRAFFE UNIQUE MODEL WATAMBULISHWA KWA WANAHABARI









KAMPUNI ya Uniqueen Entertainment inayoandaa shindano la kumsaka mwanamitindo la 'Giraffe Uniquue Model 2010' jana imeatambulisha rasmi washiriki kumi waliotinga fainali za shindano hilo litakalofanyika Desemba 24 kwenye hioteli ya Giraffe Ocean View.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Methusela Magesse alisema kwamba washiriki hao wataingia kambini Desemba 13 katika hoteli hiyo kujiandaa na shindano hilo la aina yake lenye lengo la kusaka na kuendeleza vipaji katika faini hiyo.
Alisema katika shindano hilo majaji watakuwa ni pamoja na mwanamitinmdo Victoria Martin, Mbunidfu wa mavazi Ally Remthullah, mbunifu Asia Idarious pamoja na msanii wa maigizo Steven Kanumba.
Shindano hilo limedhaminiwa na Giraffe Hotel, Global Publishers, Robialack Paints, Channel Ten na Uniqueenterz. blogspot.com.

Comments