WACHEZAJI YANGA WAGOMA




WACHEZAJI wa timu ya soka ya Yanga wamegoma kufanya mazoezi sambamba na kucheza mechi yoyote mpaka pale watakapolipwa mishahara yao na fedha zao za usajili.
Wachezaji hao walitangaza mgomo huo jioni ya leo walipokwenda katika uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mazoezi ya kawaida ya timu hiyo ambayo inajiandaa na mashindano mbalimbali.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu amethibitisha kuwepo kwa mgomo huo na kusema kuwa uongozi umesikitishwa na hatua hiyo.
Aidha, Sendeu alikiri kuwa ni kweli wachezaji hao wanadai fedha hizo ambazon zinafikia mil.75 na kusema kuwa uongozi unalifanyia kazi suala lao.

Comments