VODACOM SASA NI NUSU SHILINGI


Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Nector Foya kushoto,akifafanua namna ya utumiaji wa nusu shilingi kwa sekunde kwa waandishi wa habari mara baada ya kutangaza rasmi kwa kampuni yao kutoa huduma hiyo itakayotumiwa na wateja wake,katikati Mkuu wa udhamini wa kampuni hiyo George Rwehumbiza,kulia Afisa masoko Elihuruma Ngowi.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dares Salaam December.9.2010 Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imeboresha huduma yake ya kupiga simu na sasa wateja wa kampuni hiyo wanaweza kupiga simu kwa nusu shilingi kwa sekunde kila siku kwa kwa masaa 20.
Kabla ya mabadiliko hayo mteja wa Vodacom alikuwa akipiga simu kwa shilingi moja kwa sekunde kwa siku nzima.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nector Foya alisema Jana Jijini kwamba zaidi ya wateja milioni nane na nusu wa Vodacom watanufaika na huduma hii kwa kuongea zaidi kwa bei ile ile kwa msimu huu wa maandakizi ya sikuu.
Alisema Vodacom ina lenga kwa sasa kutoa huduma hii katika mikoa ya Tanga,Mtwara,Lindi,Zanzibar Morogoro na Dares salaam.Ikiwa na lengo la kuwawezesha wateja wake kuwasiliana zaidi na bila kikwazo chochote na hivyo kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.
“Tutaendelea kuboresha huduma zetu za mawasiliano kadri siku zinavyokwenda katika mikoa mingine ili kuhakikisha kwamba wateja wanapata huduma bora,” alisema.
Aliyashauri makundi mbalimbali katika jamii kuendelea kutumia huduma za mtandao wa Vodacom ili kuhakikisha kwamba wanajipatia maendeleo.

Licha ya kuiboresha huduma hiyo, Vodacom Tanzania inaendelea kutoa huduma nyingine za mawasiliano kama kama Nipige Tafu, Cheka Time na Vodajamaa.
Wateja wa Vodacom wanaojiunga na huduma ya Cheka Time hupata dakika za bure siku nzima kwa simu za Vodacom kwenda Vodacom wanapojisajili kwa huduma hiyo kwa shilingi 200/- hadi 2,000/-.
Hivi sasa Vodacom Tanzania ina tamba na huduma yake ya nipige tafu, ya kwanza hapa nchini ambayo ina muwezesha mteja wa Vodacom kupewa salio wakati wowote apatapo dharura iwapo simu yake haina salio.

Comments