UDE UDE KAAMUA KUJIBEBA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Sharobaro, Hamidu Hafidhi ‘Ude Ude’ baada ya kufanya kazi za kushirikishwa kwa muda mrefu sasa ameamua kuachia wimbo wake mwenyewe unaojulikana kama ‘Kujinafasi’.
Wimbo huo ameutoa katika studio za Sharobaro Records chini ya mtayarishaji, Bob Junior na video yake ameitoa kwa mtayarishaji maarufu Adam Juma.
Msanii huyu ameshafanya kazi za kushirikishwa na wasanii kama vile Ali Kiba, Hemmed, Bob Junior, Nay wa Mitego na wengine kibao.

Comments