TASWA FC KUKIPIGA NA WAANDISHI WA HABARI TOKA NCHI MBALIMBALI WALIOPO NCHINI KURIPOTI MICHUANO YA CHALENJI

VIONGOZI WA TIMU ZA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO MAJUTO OMARI (TASWA) KUSHOTO NA  FRED ALOCHO  TOKA VYOMBO VYA NJE YA NCHI WAKIZUNGUMZIA MECHI BAINA YAO ITAKAYOPIGWA JUMATATU IJAYO KWENYE UWANJA WA USTAWI WA JAMII.

HAPA WAKIPOKEA MSAADA WA TISHETI TOKA TAASISI YA KUPAMBANA NA MALARIA

WAANDISHI wa habari za michezo wa Tanzania  kupitia timu yao ya Taswa Fc watakipiga na weaandishi wa habari toka nchi za Afrika Mashariki waliopo nchini kuripoti michuano ya Tusker Chalenji jumatatu ijayo watacheza mechi ya kirafiki ikiwa na lengo la kuunga mkono kampeni za kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Mechi hiyo itapigwa kwenye viwanja vya Ustawi wa jamii ambapo viongozi wa timu hizo kila mmoja amejinadi kuwa timu yake itatoa kifua mbele siku hiyo.

Comments