SIMBA, YANGA KUFUNGA NDOA?

MSEMAJI WA SIMBA, CLIFFORD NDIMBO
MSEMAJI WA YANGA, LOUIS SENDEU

MAHASIMU wa jadi nchini vilabu vya Simba na Yanga vimeazimia kuwa kitu kimoja pindi moja ya timu ikiwa inashiriki michuano ya kimataifa.
Hata hivyo upinzani wa jadi baina yao utakuwa ukiendelea pindi timu hizo zitakapokuwa katika ligi kuu ya vodacom.
Hayo yamesema leo na wasemaji wa vilabu hiyo Louis Sendeu (Yanga) na Cliford Ndimbo (Simba) walipozungumza na waandishi wa hari.
“Wakati umefika wa kuleta mapinduzi ya soka hapa nchini wakati timu zetu zitakapopeperusha bendera ya nchi katika michuaano mbalimbali ya kimataifa. Ule wakati wa kuzisaidia timu pinzani kutoka nje ya nchi wakati wa michuano ya kimataifa uwe umemalizika, kwani mabadiliko yaliyopo hivi sasa timu inayowakilisha nchi inapoingia raundi ya tatu uwezekano wa kuongeza timu nyingine katika uwakilikishi umeongezwa,” alisema Ndimbo.
Aidha, wasemaji hao walisema ni lazima kuweka uzalendo mbele, badala ya kuwekeana fitina katika michuano ya kimataifa huku suala la upinzani katika ligi za ndani na michuano ya ndani libaki kama lililivyo.
Ikumbukwe kuwa timu hizo zina uhasimu wa jadi hapa nchini, ambapo pindi mojawapo ikishiriki michuano ya kimataifa mashabiki huamua kushangilia timu za kigeni.

Comments