NOTI MPYA ZATAMBULISHWA< KUANZA KUTUMIKA 2011


BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imetambulisha rasmi noti mpya za sh.500, 1,000, 2,000, 5,000 na 10,000 ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika mapema mwakani.
Gavana wa BOT Benno Ndulu amesema kwamba lengo la kubadili noti hizo ni kutokana na kutofanya hivyo kwa muda mrefu na mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2003.
Amesema noti zilizopo sasa zitaendelea kutumika na hizo mpya mpaka zitakapomalizika mzunguko wake.

Comments