MUSTAFA HASSANALI KUZINDUA 'KIPEPEO' MSUMBIJI, ANGOLA




MUSTAFA HASSANALI

Mbunifu wa mavazi maarufu nchini Tanzania Mustafa Hassanali, atazindua teleo jipya linalojulikana kwa jina la “KIPEPEO” tarehe 10 na 11 ya mwezi wa Disemba 2010, nchini Mozambique na Angola .
Mawazo ya jina la KIPEPEO yametokana na kisiwa cha Marashi ya karafuu Zanzibar kufuatia bustani maarufu na ya kuvutia ya Forodhani. Bustani ambayo ipo katika maeneo ya wazi , pembezoni mwa bahari ya hindi, eneo ambalo watu wa aina mbalimbali na rika tofauti hukutana kwa ajili ya chakula cha jioni na kupunga upepo wa Bahari ya Hindi. Bustani ambayo ipo jirani na jemgo maarufu la Ngome Kongwe.
Kutokana na Bustani ya Forodhani kuvutia kimandhari , watu hufurika hasa wakati wa sikukuu ya Eid ambapo Wazanzibari hujumuika pamoja wakiwa na familia zao pamoja na marafiki huku wakiwa wamevaa nguo zenye rangi tofauti tofauti, ambazo zilipelekea kuonekana kama bustani ya Eden kutokana na rangi mbalimbali za kuvutia zinafanana na mdudu kipepeo.
“Hali hii ilinivutia sana, ndipo nilipoamua toleo langu la mara hii kulipa jina la “KIPEPEO” hii imekuja kutokana na ukweli kwamba kipepeo ni mdudu ambae anavutia , hufariji, hutoa matumanini na amekuwa akionekana wazi katika mazingira yoyote kutokana na rangi zake za kuvutia”. Alieleza Mustafa Hassanali
Kipepeo ni neno la kiswahili, ambalo pia limekuwa na maana nyingine, pamoja na mdudu pia lina maana ya feni ya mokononi ambayo pia inajulikana kama feni ya mswahili, na mara nyingi imekuwa ikitumiwa na wanawake wa mwambao wa bahari.
Toleo la kipepeo litaiwakilisha Tanzania kimataifa kwa kuoneshwa kwa mara ya kwanza Luanda nchini Angola Disemba 10 katika onesho la mavazi la kibiashara (The Fashion Business Angola ) na wakati huohuo litaoneshwa tarehe 11 Disemba katika onesho la kila mwaka la wiki ya mavazi Maputo Mozambique, enesho linalojulikana kama Mozambique Fashion Week, ambalo linafanika kwa mwaka wa sita sasa.
“Natarajia kiiwakilisha Tanzania katika maonesho katika hayo ya kimataifa na kuzindua toleo la kipepeo kimataifa, katika nchi zinazozungumza lugha ya Kireno na hata nchi nyingine zilizozunguka bahari ya Hindi…. Alimalizia Hassanali.
Mwaka 2010 Mustafa Hassanali amezindua matoleo matatu, likiwemo la Parfum D’amour alizindua mwezi wa pili huko Douala , Cameroon . Karafuu , Zanzibar mwezi wa Julai na kuoneshwa tena Septemba jinini Arusha na Octoba Nairobi nchini Kenya . Na sasa ni wakati wa teleo jipya la Kipepeo litakolooneshwa kwa mara ya kwanza nchini Maputo , Mozambique na Luanda , Angola .

Comments

Post a Comment