MSHINDI GIRAFFE UNIQUE MODEL KULAMBA MILIONI !

WAKATI washiriki wa shindano la kumsaka mwanamitindo la ‘Giraffe Unique Model’ 2010 wakiingia kambini jana, mshindi wa shindano hilo ataondoka na fedha taslimu sh.milioni moja.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, mkurukenzi wa Unique Entertainment inayoandaa shindano hilo Methuselah Magese alisema pamoja na zawadi hiyo, mshindi pamoja na washiriki watakaoingia tano bora watapata mkataba wa ajira kwa mwaka mmoja katika kampuni ya rangi ya Robialac.
Alisema mshindi wa pili, wa tatu, wanne na watano kila mmoja atapata 200, 000, huku pia kutakuwa na mataji ya mabalozi wa makampuni ya Mohammed Enteprises (MeTL), na mbunifu Ally Rhemtullah ambapo kila mmoja atapata mkataba wa kazi kwa mwaka mmoja.
Wanamitindo 10 watawania taji la shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Desemba 24 kwenye hoteli ya Giraffe Ocean View, ambapo kiingilio kitakuwa sh.30,000 kwa viti maalum na 20,000 kwa viti vya kawaida.
Shindano hilo limedhaminiwa na Giraffe Ocean View Hotel, Channel 10, Global Publishers, Robbialack Paints, Ally Rhemtullah, Galacha Wear, Truworths, mtaa kwa mtaa blog na Mohammed Enterprises (MeTL).

Comments