DK REMMY ONGALA AFARIKI DUNIA

MAREHEMU DK.REMMY ONGALA ENNZI ZA UHAI WAKE
MMOJA YA WATOTO WA MAREHEMU, TOM ONGALA

MMOJA YA WATOTO WA MAREHEMU KALLY ONGALA AKISALIMIANA NA NGAZAJI WA BBC ABDALLAH MAJURA PAMOJA NA KATIBU WA TIMU ANAYOICHEZEA AZAM, NASSOR IDRISS


MMOJA YA WASANII WAKONGWE, COSMAS CHIDUMULE



KALI ONGALA
MSANII nguli wa muziki wa dansi nchini Ramazan Mtoro Ongala amefariki dunia jana baada ya kuiugua kwa muda mrefu.
Mjomba wa marehemu ambaywe pia ni msanii Mzee Makasi amesema kwamba marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa figo, moyo na shininikizo la damu.
Mipango ya mazishi inafanywa huku wakiendelea kusubiri watoto wa marehemu waliopo Dubai na London, Uingereza, pia kaka yake aliyepo nchini Congo.
Enzi za uhao wake, marehemu aliwahi kuimba nyimbo kadhaa zilizompati umaarufu ikiwemo 'Siku ya Kufa', 'Mwanza', 'Athumani' 'Kipenda Roho' , 'Mambo kwa Soksi', 'Mariamu', 'Ndumilakuwili', 'Mnyonge Ana Haki', na nyinginezo.
Aidha, Remmy aliwahi kushiri shindano la 'Mr Sura Mbaya' na kushika nafasi ya pili nyuma ya mshindi Masudi Sura Mbaya lakini alikwenda kukata rufaa akidai kuwa alistahili kunyakua ushindi.
Pia mwaka 2003 aliokoka na kuanza kuimba nyimbo za Injili na moja ya nyimbo zake ni 'Kwa Yesu kuna furaha' na 'Mbele kwa Mbele'.
Remmy aliyezaliwa mwaka 1947 huko Kinshasa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, ameacha mke Tony Ongala na watoto sita.
Mwenyezi mungu aipumzishe roho ya marehemu pema peponi, Amina

Comments