MANJU MSITA KUIWAKILISHA TANZANIA WIKI YA MAVAZI YA MSUMBIJI

 MENEJA HABARI NA MAHUSIANO WA SWAHILI FASHION WEEK SAPHIA NGALAPI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA UWAKILI WA MANJU MSITA KATIKA WIKI YA MAVAZI YA MSUMBIJI, KATIKATI  NI MANJU NA KULIA NI MENEJA MENEJA MASOKO WA  SFW HAMIS OMARY




Ni awamu ya sita kwa tamasha kubwa la kila mwaka Mozambique fashion week litakalofanyika kuanzia tarehe 6-11 Disemba mjini Maputo Msumbiji. Mahusiano kati ya Swahili na Mozambique fashion week yalianza mwaka 2009 kwa washiriki Adelia na Sheila Tique kuiwakilisha Msumbiji katika Swahili fashion week 2009 na baadaye Swahili fashion week iliwakilishwa na Jamira Vera Swai.
“Mwaka huu Marinella Rodriguez aliiwakilisha Mozambique Fashion Week katika Swahili fashion week, kwa heshima na furaha kubwa tunajivunia kumchagua Manju Msitta kuiwakilisha Swahili fashion week katika tukio muhimu mjini Maputo siku ya tarehe 11 Disemba” alisema Mustafa Hassanali muanzilishi wa Swahili Fashion Week.
“Ni furaha kubwa kuiwakilisha Tanzania na Swahili fashion week katika maonesho ya Mozambique Fashion Week mwaka huu. Nina imani nitaipeperusha vizuri bendera ya Tanzania na Afrika mashariki katika tukio hili la kidunia.” Alisema Manju msita
Manju alichaguliwa na muandaaji wa maonesho ya mavazi wa kimataifa Jan Malan Umzingeli kwa kushirikiana na Swahili Fashion Week kwa kigezo kwamba kazi zake zina kiwango cha juu kulingana na ubora wa ubunifu wa mavazi yake.
"Huu ni mwanzo wa kuimarisha mahusiano baina yetu, na sio siasa pekee inayotuunganisha Tanzania na Msumbiji ila kupitia Utamaduni pia unatuunganisha.Uhusiano huu uendelee zaidi na kuwa imara mwaka hadi mwaka.” aliongeza Hassanali.
Kwa upande mwingine Swahili fashion week itaandaa sherehe ya SIKU YA UKIMWI DUNIANI siku ya tarehe 4 Disemba katika ukumbi wa Mercury’s Zanzibar, tukio hilo limeandaliwa kwa kushirikiana na Explore Zanzibar kwa lengo la kutunisha mfuko wa ZAPHA+ (Zanzibar Association of People Living with HIV/AIDS) msherehehaji katika sherehe hiyo atakua Abby Platjees na mziki utaporomoshwa kutoka kwake DJ Eddy kutoka Zanzibar, itakua ni kusherehekea usiku mzima.
"Ni jukumu letu na kwa kila mmoja wetu na jumuiya kuleta maendeleo ya kiuchumi na jamii huku tukijua ya kwamba Swahili Fashion Week imelenga katika kuwasaidia watu waishio na virusi vya ukimwi. Kati ya jumuiya hizo Tanzania Mitindo House imekua ikipewa misaada kwa miaka 3 sasa na ni matumaini yetu kuwa tunaweza kuendelea na kufika mbele zaidi ndani ya Tanzania ” alikamilisha Hassanali.

Comments