MANJI KUZINDUA TAWI LA YANGA UHURU J'2

YUSUF MANJI

MFADHILI na mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Yanga Yusuf Manji pamoja na viongozi wengine wa klabu ya soka ya Yanga wamealikwa katika uzinduzi wa tawi kubwa la Yanga Uhuru, itakayofanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mratibu wa uzinduzi huo Kais Edwin kutoka tawi la Yanga Bomba, hafla hiyo itafanyika katika eneo lililopo tawi hilo mtaa wa Ndanda na Magila, Kariakoo jijini.
Kais alisema mbali na viongozi hao pia wamemualika mbunge wa Ilala Musa Azzan Zungu, wadau wengine pamoja na wanachama wa Yanga kwa ujumla kushiriki katika uzinduzi huo.

Comments