LADY JAYDEE AGEUKIA UJASIRIAMALI


NYOTA wa bongo fleva nchini Judith Wambura ameamua kupunguza kufanya maonyesho yake ili kujikita katika ujasiriamali.

Katika uapnde wa pili huo wa kujiongezea kipato JD ameanza kuuza maji yake yatakayojulikana kama LADY JAYDEE PURE Drinking Water, sambamba na kufungua mgahawa katika eneo la namanga.

Aidha, Jd alisema katika mapumziko hayo ya kazi za muziki atakuwa akifanya kazi zaidi nje ya nchi pamoja na kuandaa albamu yake binafsi itakayokuwa yatano tangu kuanza kwake muziki miaka kumi iliyopita.

Hata hivyo Jd anayemiliki Machozi Band alisema kuwa bendi yake itaendelea kupiga katika kumbi zake kama kawaida huku yeye atakuwa akishiriki nayo katika maonyesho yao ya siku ya ijumaa.

Comments