FIFA YAPITISHA MAJINA YA WAAMUZI 14 WA TZ

SUNDAY KAYUNI, KAIMU KATIBU MKUU WA TFF
SHIRIKISHO la soka la Kimataifa (FIFA) limepitisha majina ya waamuzi 14 kutoka Tanzania katika orodha yake ya mwaka 2011.

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni alisema waamuzi wa kati wanaume ni wane, saba wasaidizi wakati mwanamke mmoja ameteuliwa kuwa mwamuzi wa kati na wawili wasaidizi.

Kayuni aliwataja waamuzi wa kati wanaume ni pamoja na Ibada Ramadhani Kibo, Oden Mbaga Charles, Mujuni Israel na Waziri Sheha.

Wasaidizi ni Bulali Kosephat Deu, Chang’walu Hamis Ramadhani, Kanyenye Rongional John, Klemence Erasmo Jesse, Kombo Ally, Maswa Hamis na Mpenzu Samuel Hudson.

Mwamuzi wa kati mwanamke ni Gamba Judith Andrew wakati wasaidizi ni Makame Mwanahija Foum na Tibabimale Saada Hussein.

Comments

Post a Comment