CHAMA CHA MAKOCHA WA SOKA TANZANIA CHAPATA MWALIKO BRAZIL

KATIBU WA CHAMA CHA MAKOCHA WA SOKA TZ (TAFCA) EUGINE MWASAMAKI
CHAMA cha Makocha wa Soka Tanzania (TAFCA), kimepata mwaliko wa kushiriki kozi ya wiki ya masomo nchini Brazil inayotarajiwa kuanza Januari 10-25 mwakani.
Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki alisema, washiriki wa kozi hiyo wanatakiwa kujigharamia kila kitu katika mafunzo hayo.
Mwasamaki alisema, gharama za kozi hiyo ni dola 2,500 za Marekani, ambako pia washiriki wanatakiwa kujigharamia nauli na gharama nyingine wawapo huko.
Aidha Mwasamaki alisema, sambamba na kozi hiyo, kozi nyingine kama hiyo itafanyika kuanzia Julai 5-20 mwakani.
Alisema, washiriki watajifunza masuala mbalimbali ya ualimu wa soka, ambako wanaostahili kushiriki kozi hizo ni wenye sifa kuanzia ngazi ya cheti na ngazi ya kati.

Comments