CAF YAPIGA MARUFUKU WANACHAMA WAKE KUSHANGILIA KWA FATAKI, BARUTI

SUNDAY KAYUNI, KAIMU KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF)
SHIRIKISHO la Soka la Afrika (CAF) limepiga marufuku matumizi ya fataki, baruti na moto katika mechi zote inazozisimamia.
Kaimu Katibu Mkuu wa (TFF) Sunday Kayuni amesema leo kwamba maamuzi hayo yamefikiwa na kikao cha kamati ndogo ya CAF inayosimamia mashindano ya vilabu Afrika iliyokutana Novemba 12 mwaka huu nchini Tunisia.

Amesema kamati hiyo ilieleza kutoridhishwa na matumizi ya vifaa hivyo na kuviagiza vyama soka kwa nchi wanachama kushirikiana na vyombo vya usalama kuzuia matumizi yake.
Aidha, CAF, imewataka wanachama wake kuhakikisha kunakuwepo vitendea kazi na vifaa vya mawasiliano kama vile tarikishi, nakushi, mashine ya kivuli, kisoma maandishi na mchapaji wakati wa michezzo ya Shirikisho hilo ili kuwawezesha wasimamizi wa mchezo huo kutuma taarifa katika kipindi muafaka.

Comments