AZAM FC YAMNYAKUA KOCHA WA ZANZIBAR HEROES

TIMU ya soka ya Azam imemnyakua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes', Stewart John Hall kwa ajili ya kuinoa katika ligi kuu Bara.
Kwa mujibu wa habari kutoka Azam, tayari viongozi wa chama cha soka cha Zanzibar (ZFA) na Azam wameshakubalina na kinachosubiriwa ni kuingia rasmi mkataba.
Hall atarithi mikoba ya Mbrazir Amorin Itamar aliyetupiwa virago.

Comments