ABUU SEMHANDO 'BABA DIANA' WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA

PIGO jingine limetokea katika tasnia ya muziki wa dansi nchini baada ya mpiga drum wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta' Abuu Semhando maarufu kama 'Baba Diana' kufariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Marehemu alikutwa na umati baada ya kugongwa na gari eneo la Mbezi akiwa katika pikipiki yake akitokea Africana ambapo bendi yao ilikuwa inafanya onyesho usiku wa jana.
HUu ni msiba wa pili kutokea katika siku za hivi karibuni ambapo jumapili iliyopita nguli wa muziki Ramazan Mtoro Ongala alifariki kutokana na maradhi ya figo na shinikizo la damu kabla ya kuzikwa Alhamisi iliyopita.

Comments