34 WAPYA WASAJILIWA KUZICHEZEA TIMU ZA LIGI KUU BARA

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limetangaza majina ya wachezaji waliosajiliwa na timu za Ligi Kuu Tanzania bara kupitia dirisha dogo, zoezi lililoanza Novemba mosi hadi 30.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Sunday Kayuni alisema klabu 11 za Ligi Kuu ndizo zilizofanya usajili wa kujaza nafasi lakini Polisi Tanzania pekee ndio haijajaza nafasi za wachezaji kipindi hiki.
Kayuni alisema jumla ya wachezaji 34 ndio wamesajiliwa kwa ajili ya kukipiga katika kipindi cha dirisha dogo na kuwataja  wachezaji waliosajiliwa na Simba ni Meshack Abel (African Lyon) na Ali Ahmed Shiboli (KMKM), Yanga imewasajili Juma Seif Dion (JKT) na Davies Mwape (Konkola Blades), Mtibwa Sugar imemsajili Salum Swed (Azam) na Hussein Omar (Huru), JKT Ruvu imemsajili Erick Majaliwa , Bakari Kondo na Feisal Swai (Huru).
AFC : David Naftal (Simba mkopo) Majimaji imewasiliji Ulimboka Mwakingwe, Yahaya Shaban na Kassim Kilungo (Huru), Patrick Betwel (Polisi Iringa) na Mohamed Kijuso (Simba), Azam FC imemsajili Ahmad Chimpele na Ali Chimpele(U-20 Azam).
African Lyon imemsajili Shaban Aboma (Mtibwa Sugar) na John Njama (TMK Utd), Kagera Sugar imemsajili Juma Mwenza na Steven Mazunda (Huru), Toto African imewasajili Kamana Bwiza, Mussa Vologwe, Mathias Wandiba, Malegesi Mwangwa na Said Mwangwa (Huru).
Ruvu Shooting imewasajili Jumanne Ramadhani, Maneno Jasho, Lungwecha Shaibu, Omary Senkobo, Oscar Joshua, Shaban Idd, Hamis Sefu na Yasin Seleman

Comments