YANGA YAKUBALI MAPENDEKEZO YOTE YA YUSUF MANJI

MWENYEKITI WA YANGA LLOYD NCHUNGA KATIKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MCHANA WA LEO, KUSHOTO NI KATIBU MKUU LAWRANCE MWALUSAKO NA KULIA KWAKE NI MSEMAJI WA YANGA, LOUIS SENDEU

KAMATI ya utendaji ya klabu ya Yanga imekubali mapendekezo yote yaliyiotolewa na mfadhili wao Yusuf Manji.
Baadhi ya mapendekezo hayo ni pamoja na kuwepo kwa ukaguzi wa hesabu, kwenda kujinoa kwa viongozi katika chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), kufuatilia cheti cha uhamisho wa kimataifa cha mzezaji wake kutoka Ghana Kenneth Assamoh, kuimarisha kikosi chake kwa kusajili msham,buliaji wa kimataifa, mshambuliaji wa ndani ambapo mipango inafanywa kumsajili ALLY SHIBOLI kutiojka Visiwani Zanzibar.
Aidha, Yanga imeaamua kuweka kndo suala la kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani aliyehamia Azam, MMRISHO NGASSA mopaka hapo baadaye.
Pia imepanga kumuuza kwa kiasi cha shilingi milioni 100 mchezaji wake ABDI KASSIM iwapo atafaulu majaribio yake nchini Vietnam ama timu yoyote itakayomuhitaji.

Comments