YANGA :TUPO SHWARI, MSITUCHONGANISHE

MWENYEKITI WA YANGA LLOYD NCHUNGA KATIKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, KULIA KWAKE NI MSEMAJI WA YANGA LOUIS SENDEU NA KUSHOTO NI KATIBU LAWRANCE MWALUSAKO.

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga Lloyd Nchunga amesema hali ndani ya klabu hiyo ni shwari na hakuna mgogoro wowote wa chinichini unaoendelea.
Nchunga amewaambia waandishi wa habari taarifa tofauti zinazotolewa na vyombo vya habari zinawapa hofu wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo na kudhani kuwa kuna mgogoro ndani ya uongozi kitu ambacho hakina ukweli wowote.
"Yanga ipo shwari kabisa na wala hakuna tatizo lolote, jamani wanahabari msitake kutuchonganisha, acheni tuitumikie klabu yetu ili ipate mafanikio makubwa", alisema.
Baadhi ya taarifa ambazo Mwenyekiti huyo zimeonekana kumkera ni maagizio yaliyotolewa na mdjhamini wao Yusuf Manji baada ya kukutana na kocha mkuu na wachezaji wa timu hiyo na kisha kubaini baadhi ya mambo ya kiufundi zaidi.
Mambo aliyotaka Manji yafanyiwe kazi ni pamoja na kuanza kutafutwa kwa kocha mpya atakayeinoa Yanga msimu ujao kwani kocha wa sasa Kostadi n Papic uwezo wake hauridhishi hivyo ataondoka mara baada ya nmzunguko wa pili wa ligi kumalizika.
Kama hiyo haitoshi pia Manji amehoji matumizi ya shilingi bilioni 1 zilizoingia katika uongozi huo katika siku 100 kiasi cha kushindwa hata kutatua baadhi ya matatizo ikiwemo kumpa dola 3000 za matibabu mchezaji wake Haruna Shamte.

Comments