VIINGILIO MICHUANO YA CECAFA TUSKER CHALENGE VYAFUTWA



BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limefuta viingilio vya mashindano hayo kuanzia leo hadi Jumamosi kwa sababu ya ufinyu wa watazamaji wanaojitokeza kuishuhudia.
 Rais wa CECAFA, Leodegar Tenga alisema, pamoja na kuondoa viingilio, lakini VIP A, B na C hazirusiwi kwa watakaoingia uwanjani na kuwaasa mashabiki kuingia na bendera za timu watakazoshangilia.
Tenga alisema, hatua ya kuhamasisha wadau kuingia bure viwanjani, imetokana na wadhamini wa mashindano hayo Kampuni ya bia ya Afrika Mashariki, kupitia bia ya Tusker kuwataka waandaaji wa mashindano hayo kutoa wito kwa watazamaji kujitokeza uwanjani.
Aliongeza kuwa, hatua hiyo pia itasaidia wadau wa soka hapa nchini kujifunza mbinu za timu nyingine za nje ambazo soka lao liko juu.

Comments