SIMBA YAMTEUA PATRICK PHIRI KUWA MKURUGENZI WA BENCHI LA UFUNDI

ISMAIL ADEN RAGE, MWENYEKITI WA SIMBA

KAMATI ya utendaji ya klabu ya Simba imeamua kumuongezea mkataba aliyekuwa Kocha mkuu wake Patrick Phiri na kumpandisha cheo kuwa Mkurugenzi wa Ufundi.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, alisema uamuzi huo umepitishwa na kamati ya utendaji iliyoketi juzi Jumatano.
Alisema kuwa kamati hiyo mbali ya kumpa ulaji huo Phiri lakini pia imeunda kamati ya ufundi ambayo itakuwa na watu wanane.
“Kumekuwa na maneno mengi yanasemwa juu ya Kocha wetu, Patrick Phiri, lakini nataka kuwafahamisha kuwa, Kamati ya utendaji iliyoketi jana ‘juzi’,” alisema na kuongeza.
“Aidha Kamati ya utendaji pia imemteua Phiri kuwa Mkurugenzi wa ufundi badala ya Kocha, hii ni kutokana na uongozi wetu kufanya mabadiliko ya mfumo wa kiuongozi,” alisema.
Aliwataja kuwa ni, Ibrahim Masoud (mwenyekiti), Evodius Mtawala (katibu), wakati wajumbe ni, Saidi Tulli, Khalid Abeid, Arthur Mwambeta, Abdallah Kibaden, Patrick Phiri na Dan Manembe.
Rage alisema kuwa, kutokana na kuukubali uwezo wa Kibaden, wamepanga kumuajiri na atakuwa Mkurugenzi wa ufundi wa timu za vijana, akiwa na jukumu la kuibua vipaji na atavinoa vikosi vya vijana chini ya miaka 17 na 14.

Comments