SIMBA YAIINGIZA MJINI YANGA, YANYAKUA KIFAA ILICHOKUWA IKIKIWANIA KUTOKA ZENJI

KIKOSI CHA SIMBA

SIMBA imewazidi kete mahasimu wao wa jadi nchini Yanga baada ya kufanikiwa kumsajili mshambuliaji kutoka wa timu ya Mundu na Timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ Ali Ahmed maarufu kama ‘Shiboli’.

Juzi mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga alisema klabu yake ipo katika mipango ya kumsajili mchezaji huyo kwa ajili ya kuichezea timu yao.
Hatua ya Simba inakamilisha mazungumzo baina ya uongozi wa timu hizo kabla ya mchezahi huyo kusaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo.
Makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ alisema jana kwamba mchezaji huyo ameingia mkataba wa miaka mitatu.
Kaburu alisema wanaamini uwepo wa mchezaji huo utaongeza chachu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo na hivyo kuiletea mafanikio klabu hiyo.
Alisema, mbali na mchezaji huyo uongozi upo katika mazungumzo na wachezaji kadhaa ambao itawasajili kuichezea timu hiyo katika mzunguko wa pili wa ligi kuu bara na mashindano ya kimataifa.
“Sisi tunafanya usajili wetu kiufundi zaidi, hatutaki kukurupuka kwa kusajili wachezaji wa kujaza timu, tunataka wachezaji wa kuichezea Simba kwa faida”, Alisema Kaburu.

Comments