SIMBA, AZAM KUKIPIGA U/UHURU JMOSI

TIMU za Simba na Azam zinatarajiwa kumenyana jumamosi hii katika uwanja wa Uhuru ikiwa ni mechi maalum ya sehemu ya tamasha kubwa la michezo na burudani la AMKA KIJANA.
Lengo la tamasha hilo ni kuwahamasisha vijana waamke na kujua umuhimu wao katika jamii ikiwa ni pamoja na kusaidia maendeleo katika nyanja mbalimbali.
Katika tamasha hilo pia kutakuwa na burudani toka kwasanii mbalimbali watakaotumbuiza wakiwemo kundi la TMK WANAUME FAMILY, TIP TOP CONNECTION, BERRY BLACK, MB DOG, OMARY OMARY, AT, ABUU FLEVAM, MUUMIN MWINJUMA NA BENDI YAKE YA BWAGAMOYO SOUND.

Comments