SHINDANO LA KISURA WA TANZANIA 2010 LAZINDULIWA RASMI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MCHAKATO wa kumpata Kisura wa Tanzania 2010/11, unatarajia kuanza Desemba 11 mwaka huu mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti na mwanzilishi wa kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), Juliana Urio alisema hatua ya kwanza ya usahili  huo, mbali na Mkoa wa Mwanza, pia itahusisha mikoa ya Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora na Dar es Salaam, Arusha, Karatu, Dodoma, Iringa, Mbeya na Songea

Alisema kuwa timu ya BTA ikiambatana na Mwanamitindo chipukizi Kemmy Kalikawe wanatarajiwa kuondoka jijini Dar es Salaam Desemba 10 kwenda Mwanza kuanza usahili  huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake.

Alisema kuwa mbali ya mchujo kwa wasichana wenye sifa zinazotakiwa katika shindano hilo, pia wasichana hao watakaoshiriki kwenye mchujo watapewa mafunzo juu ya janga la Ukimwi na Virusi vyake (HIV),

Ms. Urio alisema kuwa mchujo kwa wasichana wa Mwanza utafanyika Desemba 11 hadi 12 kabla ya usahili huo kuhamia Musoma (Mara) ambapo watafanya mchujo Desemba 13 hadi 14.

“Desemba 15 itakuwa ni zamu ya wasichana wa mkoani Kagera ambapo mchujo utafanyika kwa siku moja na Desemba 16 Timu ya BTA itaelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuendelea na usahili huo,” alisema Ms. Urio.

Aliongeza: “Desemba 17 timu ya BTA itaelekea mkoani Tabora kuendelea na mchujo huo na baada ya hapo msafara huo utarejea Dar es Salaam kwa ajili ya usahili huo utakaofanyika jijini humo kwa siku mbili, yaani kuanzia Desemba 19 hadi 20 siku ambayo ndiyo mwisho wa hatua ya kwanza ya usahili huo.”

Ms. Urio alisema kuwa hatua ya pili ya usahili huo (Phase II), itafanyika katika mikoa ya Arusha, Karatu na Dodoma kuanzia Desemba 21 hadi 29.

Alisema kuwa Desemba 22 mchujo huo utaanzia katika Mkoa wa Arusha na kufanyika kwa siku mbili kabla ya kuhamia Dodoma Desemba 27 hadi 29, hiyo ikiwa ndiyo mwisho wa hatua ya pili.

Alisema kuwa hatua ya tatu ya mchakato huo itahusisha mikoa ya Iringa, Mbeya na Ruvuma kuanzia Januari 2 hadi 4 mwaka 2011 watakuwa Mkoa wa Iringa.

“Januari 4 msafara wa BTA utahamia Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya mchujo utakaofanyika kwa siku moja na kwamba Januari 6 usahili huo utahamia mjini Songea, mkoani Ruvuma ambapo utafanyika kwa siku moja pia.

“Januari 8, 2011 itakuwa ndio mwisho wa mchakato huo wa mchujo wa kumtafuta Kisura wa Tanzania 2010/11. Ms. Urio alisema usahili huo utaonyeshwa katika kituo cha Televisheni cha TBC1.

Aliongeza: “Fainali za mashindano hayo yanatarajiwa kuwa Machi 2011 katika ukumbi utakaotangazwa hapo baadaye.”

Taji la Kisura wa Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Diana Ibrahim kutoka Mkoa wa Mara.

Ms. Urio aliongezea akisema, pamoja na kuwa shindano zima linahusu kumtafuta mwanamitindo wa kimataifa vile vile lengo kuu la shindano la Kisura wa Tanzania ni:-
•    kuwajengea uwezo watoto wa kike katika elimu iliyo rasmi na isiyo rasmi;
•    kuwafundisha masuala ya uzazi, afya, pamoja na jinsi ya kujikinga na magonjwa hasa ugonjwa wa ukimwi;
•    kuwafundisha ujasiriamali;
•    kuwajengea uwezo katika masuala ya uongozi ili waweze kuwa viongozi watakao leta mabadiliko katika jamii na taifa kwa ujumla.

Mdhamini mkuu wa shindano la Kisura wa Tanzania 2010/11 ni Family Health International (FHI), na wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort Hotel, TanFoam (Arusha), SBC Tanzania Limited, Flare Magazine na Hugo Domingo.

Comments