KILIMANJARO STARS KUKIPIGA NA HARAMBEE NOVEMBA 21



KAIMU KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF) SUNDAY KAYUNI

TIMU ya Soka ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ Novemba 21, mchezo utkaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi kwa timu hizo katika michuano ya kombe la Tusker inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 27 hadi Desemba 11 mwaka huu nchini Tanzania.
Stars ipo kambini ikiendelea kujiandaa na michuano hiyo inayotarajia kuzishirikisha pia Uganda, Zambia, Malawi na Ethiopia.

Comments