HOTELI YA SOUTHERN SUN KUTOA ZAWADI YA GAUNI BORA KATIKA SWAHILI FASHION WEEK

BAADHI YA WABUNIFU WA MAVAZI WANAOTARAJIA KUSHIRIKI MAONYESHO YA MAVAZI YA SWAHILI FASHION WEEK



WAKATI maonyesho ya tatu ya mitindo na mavazi ya Swahili Fashion Week kwa mwaka 2010 yakianza usiku wa leo katika viwanja vya Karimjee, hoteli ya Southern Sun itatoa zawadi kwa gauni litakalokuwa bora zaidi kati ya yale yatakayoshirikishikishwa kwenye maonyesho hayo.

Meneja mkuu wa hoteli hiyo Adam Fuller alisema kwamba lengo la kutoa zawadi hiyo ni kusaidia kukuza sanaa ya ubunifu hapa nchini sambamba na kuleta changamoto kwa wabunifu kuandaa kazi zilizo bora zaidi zitakazoleta ushindani katika soko la nje.
Alisema hoteli yake inajivunia kutoa mchango wake katika tasnia hiyo ya sanaa na ubunifu wa mavazi Afrika tangua kuanza kwa maonyesho hayo miaka miwili iliyopita.
Wabunifu 24 wa mavazi kutoka nchi za Afrika hasa zile zinazoongea lugha ya Kiswahili wapo nchini tayari kwa maonyesho hayo yatakayomalizika kesho huku yakiambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo warsha toka kwa washiriki wa maonyesho hayo yaliyoandaliwa na mbunifu maarufu wa mavazi nchini Mustafa Hassanali huku mwaka huu yakifanyik kwa mara ya tatu.
Wabunifu wanaotarajiwa kuonyesha kazi zao ni pamoja na Manju Msita, Ailinda Sawe, Farha Sultan, Kemi Kalikawe, Asia Idarous, Jamila Vera Swai, Tanzania Mitindo Haouse, Robi Moro, Zamda George, Chichi London, Khadija Mwanamboka, Made By Afrika, Gabriel Mollel na Shelina Ibrahim, kutoka Tanzania, Sonu Sharma, Kooroo, Moo Cow, Kiko Romeo na John Kaveke kutoka Kenya.
Pia wamo Mafi Designs (Ethiopia), Asos Africa (UK)Stella Attal (Uganda), Marinella Rodriguez (Msumbiji) na wengine.
Maonyesho hayo yamedhaminiwa na Home of Swahili Fashion Week, Southern Sun, Origin Africa, Usaid Compete, Malaria Haikubaliki, Baraza la Sanaa Tanzania, Colour Print, Darling Hair, Global Outdoor, Nipashe, Klabu Bilicanas, Sengi Tours, Ultimate Security, Monier 2000, Amarula, Vayle Springs, ZG Films na wengineo

Comments