HALI YA HEWA YACHAFUKA KLABU YA YANGA

MAKAMU MWENYEKITI WA YANGA, DAVIES MOSHA

WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA YANGA KATIKA PICHA PAMOJA NA MDHAMINI WAO YUSUF MANJI WATATU KUTOKA KULIA WALIOSIMAMA NA ALIYEKUWA MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI, RIDHWAN KIKWETE MARA BAADA YA KUCHAGULIWA JULAI 18.

HALI si shwari ndani ya klabu ya Yanga baada ya kuwepo kwa msigano baina ya mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga na Makamu wake Davies Mosha kiasi cha kumfanya Mosha aamue kujiweka kando katika masuala ya kuiongoza klabu hiyo.
Sababu za kujiweka kando kwa Mosha zinatokana na Nchunga kupiga marufuku kiongozi yoyote kuzungumza na waandishi wa habari zaidi yake na Katibu Mkuu na kiongozi yoyote atakayekiuka amri hiyo atachukuliwa hatua za kinidhamu.
Mosha amesema hawezi kufanya kazi kibubu bubu sababu majukumu aliyonayo yanahitaji kuwapa taarifa wanachama na taarifa hizo zitapatikana kupitia vyombo vya habari.
Baada ya msimamo huo wa Mosha, Nchunga alitaka kuweka mambo sawa kwa kumuita Mosha lakini makamu huyo aligoma na kudai kuwa kuna masuala mengi ya msingi aliyoyahoji kupitia kikao cha kamati ya utendaji na mfadhili wao mapema wiki hii ambayo Nchunga alipaswa kuweka wazi.

Comments