BONDIA WATZ ASHRAF SULEIMAN ATWAA UBINGWA DUNIA WA MCHEZO WA RAZMAVARAN, HUKO IRAN



MASHINDANO YA UBINGWA WA DUNIA WA MCHEZO WA RAZMAVARAN.( 4 - 6 NOVEMBA 2010 ) KUPITIA SHIRIKISHO LA MASUMBWI LA TANZANIA ( PST ) TANZANIA ILIWAKILISHWA NA MABONDIA WAWILI.
ASHRAF SULEIMAN WA ZANZIBAR ALIYEPATA MEDALI YA FEDHA BAADA YA KUTOA PERZMAN KORDBAHMAN WA IRAN KWENYE NUSU FAINALI LAKINI AKASHINDWA KATIKA FAINALI KWA KUDUNDWA NA MOHSEN SHIRIAN WA IRAN AMBAYE ALIMTOA JASON ZACK WA AUTRALIA KWENYE NUSU FAINALI.
SAID JEBA WA TANGA ALISHINDWA NUSU FAINALI NA MORTAZA AZIMI WA IRAN LAKINI AKAMSHINDA KIUFUNDI TIAO WA NEW ZEALAND KATIKA KUWANIA NAFASI YA TATU NA HIVYO KUTWAA MEDALI YA SHABA.
HII NI MARA YA KWANZA KWA TANZANIA KUSHIRIKI MASHINDANO YA SANAA HII YA KUPIGANA YENYE ASILI YA IRAN AMBAYO SIYO KICKBOXING WALA KARATE WALA BOXING BALI NI RAZMAVARAN.
KUTOKANA NA USHINDI WA ASHRAF SULEIMAN TANZANIA ITASHIRIKI KWANYE MASHINDANO YAJAYO YA MCHEZO HUU AMBAYO HUDHAMINIWA NA SERIKALI YA IRAN KUPITIA KWA PROMOTA WA MASUMBWI AMIR RAJANDAR AMBAYE ALIKUWA BINGWA WA DUNIA WA MUAYTHAI.
AIDHA PST ITAPELEKA IRAN WAAMUZI WAWILI KWENDA KUJIFUNZA UAMUZI WA RAZMAVARAN .
TIMU ILIONDOKA JUMATATU TAREHE 1 NOVEMBA 2010 NA KURUDI TANZANIA JUMANNE TAREHE 9 NOV 2010.
ASANTE,
EMMANUEL MLUNDWA

Comments