BASATA YAPONGEZA MAOFISA UTAMADUNI KUFUATIA UTULIVU SIKUKUU YA EID EL HAJJ

KATIBU MTENDAJI WA BASATA, GHONCHE MATEREGO
Baraza la Sanaa la Taifa kwa niaba ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo (WHUM) linapenda kuwapongeza Maafisa Utamaduni wote kushamirisha sikukuu ya Eid El Haji kusherehekewa kwa utulivu na amani. Itakumbukwa tarehe 20/09/2010, Serikali kupitia Katibu Mkuu wa WHUM Bw. Seth Kamuhanda ilitoa tamko Kwa maafisa utamaduni kutotoa vibali vya kuendesha Disco Toto kwa kumbi ambazo si salama na zisizo na vibali. Tamko hilo liliweka msisitizo kwa kumbi zote za sanaa na burudani kuhakikisha zinafanyiwa marekebisho ya kiusalama na kusajiliwa kabla ya tarehe 31/12/2010. Serikali inasisitiza kwamba, yeyote atakayekiuka agizo hilo ukumbi wake utafungiwa. Hadi sasa hatujapokea taarifa yoyote mbaya kutokana na Sherehe za Eid El Hajj.

Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI – BASATA

Comments