ALL STARS VS NYOTA ZENJI KUWAPONGEZA RAIS KIKWETE NA DK.SHEIN

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA< MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE.

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR< DK> ALI  MOHAMMED SHEIN.

Kampuni ya Vanedrick imeandaa mechi ya kumpongeza Rais wa Dkt. Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dkt. Ally Mohammed Shein pamoja na Wabunge wa vyama vyote vya siasa kwa kuchaguliwa kuingia bungeni.
Mratibu Xavier Mhagama alisema kwamba medhi hiyo iNATARAJIWA  kuchezwa Novemba 21 katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kwa kuzikutanisha Dar es Salaam All Stars pamoja na timu inayoundwa na nyota kutoka visiwani Zanzibar
Kocha wa timu ya nyota wa Dar es Salaam Jamhuri Kihwelu 'Julio' amekitaja kikosi chake ambacho kitaingia kambini jumatano ijayo katika hoteli ya Lamada iliyopo Ilala Dar es Salaam ambako watakaa hadi siku ya mechi kuwa kitaundwa na Simba) na Ivo Mapunda (African Lyon),Freddy Mbuna (Yanga), Jabu Juma (Simba), Meshark Abel (African Lyon), Haruna Moshi Boban (Mchezaji Huru), Rashid Gumbo, (Simba), Ibrahim Mwaipopo (Azam FC), Juma Seif (JKT Ruvu) na Salum Abubakar (Azam FC).
Wengine ni Monja Liseki (Mtibwa Sugar ), Nsa Job (Yanga), Pius Kasambale (JKT Ruvu), Himid Mao (Azam FC), Amri Kiemba,  Mohamed Kijuso, Mussa Mgosi (Simba), Jerson Tegete (Yanga), Adam Kingwande (African Lyon), Athuman Iddy Chuji (Yanga), Kelvin Yondani (Simba) , Kally Ongala, Salum Swedi na Ramadhan Chombo a.k.a Ridondo  wote toka Azam FC.
Mara baada ya kutaja kikosi hicho Jamhuri amesisitiza kuwa Danny Mrwanda anayesakata kabumbu nchini Vietnam atatua nchini ili kuongeza nguvu huku timu ya Zanzibar wakitarajiwa kuwasili Novemba 19.
Meneja wa timu hiyo ni Mkurugenzi wa Kampuni ya MUZASHA , Muzamil Katunzi.



Mhadama alitaja viingilio katika mechi hiyo kuwa ni Jukwaa Kuu sh.10,000 Jukwaa la Kijani sh.8,000 na mzunguko ni sh.3,000.

Comments