WAKAZI WA MUSOMA KUSHUHUDIA MECHI BAINA YA SIMBA DHIDI YA ULINZI YA KENYA

WEKUNDU WA MSIMBAZI
MABINGWA watetezi wa ligi Kuu Bara timu ya soka ya Simba imeondoka jijini Dar es Salaam kwenda Tabora kwa ajili ya kambi maalum huku ikiwaacha nyota wake saba wakiwemo mshambuliaji wake wa kimataifa Patrick Ochan kutoka Uganda na Kiungo Hillary Echessa kutoka Kenya.
Ofisa habari wa Simba Clifford Ndimbo alisema aliwataja wachezaji wengine walioachwa ni pamoja na mshambuliaji wake mahiri Mussa Hassan Mgosi na nahodha wa timu hiyo Nico Nyagawa, Uhuru Seleman na Salum Kanoni wameachwa kutokana na kuwa wagonjwa ambapo wanatarajiwa kukutana na daktari kesho.
Alisema katika safari hiyo pia hakuhusishwa kipa wake Mohammed Aziz, pamoja, Joseph Owino ambaye amekwenda Kenya kuitumikia timu ya Taifa, pamoja na wachezaji Mohammed Banka, Juma Kaseja na Haruna Shamte ambao wapo timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ inayojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Morocco, Oktoba 9.
Simba imekwenda mkoani humo kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na mechi yake ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya watani wake wa jadi yanga inayotarajiwa kupigwa Oktoba 16 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Ndimbo alisema ikiwa mkoani Tabora kesho inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na Rhino ya huko kabla alhamis kwenda Mwanza na kisha jumapili itakwenda mjini Musoma ambapo jumatatu ijayo itacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki na Ulinzi ya Kenya mchezo utakaopigwa katika mji wa Shiratu.
“Baada ya mechi na Ulinzi timu itarudi Mwanza siku ya Jumanne ili kuendelea na kuajiandaa na mechi yetu dhidi ya Yanga”, Alisema Ndimbo.

Comments