SWAHILI FASHION WEEK KUZINDULIWA MUCH MORE LEO

HAFLA maalum ya uzinduzi wa maonyesho ya tatu ya wiki ya mavazi ya kiswahili 'Swahili Fashion Week' inafanyika usiku wa leo katika ukumbi wa Much More uliopo ndani ya klabu Bilicanas jijini Dar es Salaam.
Mwandaaji wa maonyesho hayo Mustafa Hassanali amesema kwamba kupitia hafla ya leo wabunifu mbalimbali wa mavazi na mitindo, warembo na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo watakaoshiriki katika wiki hiyo watapata fursa ya kushuhudia uzinduzi huo.
Swahili Fashion Week itafanyika Novemba 4 hadi 6 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo wabunifu wa mavazi 24 wataonyesha kazi zao.

Comments