SERIKALI YATAKA TFF ICHUKUE HATUA KALI KWA UZEMBE ULIOTOKANA NA KUKATIKA KWA WIMBO WA TAIFA SIKU YA MECHI KATI YA STARS NA MOROCCO

KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO, SETH KAMUHANDA AKITOA TAMKO LA SERIKALI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO KUHUSIANA NA KUKATIKA KWA WIMBO WA TAIFA SIKU YA MECHI KATI YA STARS NA MOROCCO, KULIA KWAKE MKURUGENZI WA MICHEZO, LEONARD THADEO
SAKATA la kutopigwa kwa nyimbo za Taifa katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki kombe la Mataifa ya Afrika kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Morocco limechukua sura mpya baada ya Serikali kujitoa katika sakata hilo na kulitaka Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kulishughulikia ipasavyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Seth Kamuhanda alisema alitoa masharti kwa TFF kuhakikisha kwamba kuanzia sasa katika kila mchezo wa Kimataifa unaofanyika hapa Tanzania ni pamoja na kuimbwa kwa nyimbo za Taifa kwa bendi za majeshi ‘brass band’ kama ilivyokuwa ikifanyika miaka iliyopita.
Kamuhanda alisema Serikali imeleekeza TFF kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kufanya uzembe na kulitia aibu kubwa taifa ambako wao wametoa kauli ya kutohusika na tukio lile kwa sababu taratibu zile zilielekezwa kwa TFF.
Aidha kuhusu matumizi ya vyoo vilivyoko katika uwanja wa Taifa, Kamuhanda alisema watalifanyia kazi ingawa Mkurugenzi wa Michezo, Leonald Thadeo alieleza kwamba katika mchezo wa juzi ulifanyika.

Comments