RAGE:SIWEZI KUSHINDANA NA KUDRA ZA MWENYEZI MUNGU

ALHAJ ISMAIL ADEN RAGE

MWENYEKITI wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema yeye ni AL Hajj hivyo hawezi kushindana na kudra za Mwenyezi Mungu.
Kauli hiyo ya Rage inafuata baadhi ya wanachama kulalamika kuwa timu hiyo ilifungwa kutokana na mwenyekiti hiyo kuipa kisogo timu hiyo na kuelekeza nguvu zake kwenye kampeni akiwa anagombea ubunge wa Jimbo la Tabora Mjini kwa tiketi ya CCM.
Hiyo inatokana an Simba kufungwa bao 1-0 na mahasimu wao wa jadi Yanga jumamosi iliyopita, katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Akizungumza nami kwa njia ya simu kutoka Tabora jana alisema ameshiriki kikamilifu katika maandalizi ya mechi hiyo kwani alikiweka kambini kikosi cha timu hiyo mkoani Tabora kwa karibu siku tatu ambapo pamoja na mazoezi aliongea na wachezaji na kuwajenga kisaikolojia.
Alisema watu wasioukbali matokeo hayo si wanamichezo kwanmi katika soka kuna kushinda, kushindwa na kutoka sare hivyo matokeo hayo ni sehemu ya mchezo.
"Walitoklewa Brazil na Ujeruman katika kombe la dunia ije kuwa Simba kufungwa bao 1 na Yanga, mie nadhani kuna watu wanataka kutuvuruga wanasimba ili tupoteze mwelekeo kabisa katika ligi hii, haitawezekana kwani Simba ipo pamoja na ushindi wa msimu huu utakakuwepo kama ilivyoada", Alisema.
Kama hiyo haitoshi Rage alisema kuwa pamoja na kufungwa huko timu yake ilicheza vizuri sana lakini walikuwa na bahati mbaya siku hiyo na hasa ikizingatiwa kuwa nafasi sita walizopata walishindwa kuzitumia vema lakini wenzao nafasi moja waliyoipata walitumia vizuri.

Comments