MUSA MGOSI ATEMWA TAIFA STARS

MUSA HASSAN MGOSI

KOCHA mkuu wa timu ya timu ya Taifa 'Taifa Stars', Jan Paulsen amemtema katika kikosi hicho mshambuliji wa timu hiyo Mussa Hassan Mgosi kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti..
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Florian Kaijage, alisema uamuzi huo umehusisha pia daktari wa timu hiyo.
Kaijage alisema  baada ya daktari uchunguzu wa daktari ilionekana kuwa Mgosi hatoweza kucheza mechi ya kuwania kucheza fainali za mataifa ya Afrika baina ya Stars na Morocco itakayopigwa  Oktoba 9, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kutemwa kwa Mgossi kocha Poulsen hataziba nafasi yake badala yake atabakia na nyota 22 kwa maandalizi ya hiyo ya pili katika kampeni hizo zitakazofanyika mwaka 2012 nchini Gabon na Guinea ya Ikweta.
Stars italazimika kushinda ili kuhuisha matumaini ya kucheza fainali hizo kwa mara ya pili baada ya kushiriki fainali hizo mara moja pekee 1980, mjini Lagos, Nigeria.
Timu hizo zitakutana siku hiyo huku kila moja ikiwa na pointi moja kwani wakati Stars ikivuna sare ya bao 1-1 ya ugenini dhidi ya Algeria, Morocco ilivuna sare ya nyumbani ya bila kufungana na Afrika ya Kati.
Aidha, Kaijage alisema nyota wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi Nizar Halfan, Henry Joseph, Idrisa Rajabu wanatarajiwa kuripoti wakati wowote.

Comments