MALARIA HAIKUBALIKI YAPIGA HODI SWAHILI FASHION WEEK 2010

MENEJA HABARI NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA VOICE 11 UNAOFANYA KAZI CHINI YA MPANGO WA MALARIA HAIKUBALIKI, FAUZIYAT ABOOD AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI) KUHUSIANA NA USHIRIKI WAO KATIKA SWAHILI FASHION WEEK


WABUNIFU WATATU WATAKAOONYESHA MAVAZI CHINI YA MALARIA HAIKUBALIKI KUTOKA KUSHOTO FRANSICA (FRANCO DESIGN), SALIM ALLY (MTOKO DESIGN), PAMOJA NA DIANA MAGESE WAKIWA NA FAUZIYAT.

MRADI wa kupambambana na Malaria Voices 11 umejitokeza kuchangia katika wiki ya mavazi ya kiswahili ‘Swahili Fashion Week 2010’ ambapo wabunifu wake watatu watashiriki katika kuonyesha mavazi kwenye wiki hiyo itakayoanzxa Novemba 4 hadi 6 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Much More uliopo ndani ya klabu Bilicanas Meneja Habari na Utetezi wa mradi huo Fauziyat Abood alisema kwamba wameamua kushiriki katika tukia hilo wakiamini kwamba wataweza kufikisha ujumbe kwa Watanzania kwa namna moja ama nyingine na hasa ikizingatiwa wapo katika kampeni ya kitaifa ya kupambana na Malaria nchini.
Alisema kupitia maonyesho hayo wabunifu watatu Mtoko Design, Francisca Shirima na Diana Magesa ambao wataonyesha mavazi yao waliyoyabuni ambayo kwa hakika yatafikisha ujumbe kwa kwatu mbalimbali ambao watajitokeza katika wiki hiyo.
“Wabunifu hao wameandaa mavazi ambayo yatatoa picha halisi ya kampeni ya Malaria Haikubaliki, hii ni mara yao ya kwanza kushiriki katika jukwaa bora la maonyesho ya mavazi katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa hisani ya Malaria Haikubaliki”, Alisema Fauziyat.
Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya kiswahili ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maeneo hayo.
Wabunifu watakaoonesha mavazi katika Swahili Fashion Week kwa mwaka huu ni pamoja na Ailinda Sawe, Manju Msita, Kemi Kalikawe, Christine Mhando, Shellina Ibrahim, Farha Naaz Sultan, Gabriel Mollel, Robi Morro, Asia Idarous, Zamda George, Khadija Mwanamboka, Jamilla Vera Swai and Made by Afrika. wabunifu kutoka Kenya ni Sonu Sharma, Moo Cow, KiKoromeo, John Kavike na Kooroo, na kutoka Uganda ni mbunifu Stella Atal.
Mbali na maonyesho hayo pia kutakuwepo aina tofauti za burudani kutoka kwa vikundi mbalimbali vya muziki, uchoraji wa hina, usukaji mikeka, sambamba na semina za aina tofauti zitakazo washirikisha wabunifu wa mavazi, huku pia kutakuwa za zawadi mbalimbali zitakazotolewa mwaka huu kwa lengo la kutambua na kuthamini vipaji vya aina mbalimbali vitakavyooneshwa, ikiwa ni pamoja na zawadi ya mwaka kwa mbunifu anaechipukia
Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na Home of Swahili Fashion week Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, EATV, East Africa Radio, Malaria Haikubaliki, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery LTD, 1 & 1 internet solutions, Sengi Tours, Ifashion na 361 Degrees.

Comments

  1. `Swahili fashion'...??! Oh, aaah, `maonyesho ya waswahili' au...haijakolea, maonyesho kuhusu nini?....ndio kuhusu mavazi, kwahiyo `maonyesho ya waswahili ya mavazi'...mmmh mbona inakuwa ndfu sana, ok, labdandio maana ikaitwa `swahili fashion' kazi kelikweli!

    ReplyDelete

Post a Comment