MAANDALIZI YA SENSA YA TAIFA YALIVYOFANYIKA MKOANI SINGIDA

Mtaalam wa ramani kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu Jesse Munissi, akiwajibika kwa kuingiza mipaka ya ramani na adadi ya vituo kwa ajili ya sensa katika ramani ya Mkoa wa Singida


Kiongozi ya timu ya wataalamu wa kupima ramani na mipaka kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu, Francis Changarawe, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hivi karibuni Mkoani Singida.
 
Kutoka kulia ni mpima mipaka na ramani kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu, Deusdedith Byorushengo, Amon Komba(katikati) wakipata maelezo ya mipaka ya kijiji kutoka kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Iyumbu Wilayani Ikungi, Emmanuel Nyasa

Meneja wa Takwimu Mkoa wa Singida Nestory Mazinza, akitoa maelezo kuhusu maandalizi ya sensa na upimaji wa mipaka na vituo mkoani humo.

MAANDALIZI ya Sensa ya Taifa ya mwaka 2012, yameaanza nchini kwa kuanza kutambua mipaka na kugawa maeneo ya vituo vya kuhesabia watu katika mikoa mbalimbali.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Meneja wa Takwimu Mkoa wa Singida, Nestory Mazinza, na kusema hivi sasa ofisi ya Taifa ya Takwimu imesambaza wataalamu wake wa kupima ramani katika maeneo ya mkoa huo.
Alisema kwa kutambua umuhimu wa Sensa ya Taifa, wameanza na kupima mipaka ya vijiji na vitongoji ambavyo vitakuwa dira ya kupata idadi ya vituo vya kuhesabia watu.
“Sensa ni maandalizi nasi kwa kulitambua hilo tumejipanga na kwa hatua za awali kupitia ofisi yetu ya Takwimu ya Taifa, tayari tumeanza kupima ramani kuanzia ngazi ya vijiji na vitongoji ili kujua idadiya kaya ambayo itatusaidia kupanga idadi ya vituo vya kuhesabia watu” alisema Mazinza
Aidha alisema kwa Mkoa wa Singida wamefanikiwa kupima ramani katikaWilaya za Iramba, Ikungi, Manyoni na ifikapo Octoba 15, wataanza na Wilaya ya Singida mjini.
Alisema katika hatua hiyo wamekuwa kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa na halmashauri zote kwa kuwapa taarifa za zoezi la upimaji wa mipaka ya ramani wenyeviti na watendaji wa vijiji.
“Unajua bila kuwa na maandalizi mazuri na ya uhakika na kuliona hilo tunahitaji sensa ijayoya mwaka 2012, iwe ya kisasa kwa kuwa na mippaka yote muhimu ambayo itawasaidia waalamu wa kuhesabu watu kutopata shida katika maeneo watakayo pangiwa” alisema Mazinza
Hata hivyo Meneja huyo alisema hivi sasa wamejipanga kukabiliana na changamoto ya kuhakikisha wanafika kila kona ya kijiji na kitongoji ili kuwa na takwimu ambazo zitasaidia chochea kwa haraka miradi ya maendeleo katika mkoa wa singida na Taifa kwa ujumla.
Zoezi la upimaji wa mipaka ya ramani kwa ajili ya maandalizi ya sensa ya mwaka 2012, tayari limeshafanyi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Pwani, Manyara na hivi sasa lipo mikoa ya Singida na Lindi.

Comments