KONYAGI YAIDHAMINI MWANZA UNITED

MENEJA WA KINYWAJI CHA KONYAGI MARTHA BANGU KATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA UDHAMINI WA KINYWAJI HICHO KWA TIMU YA MWANZA UNITED, KULIA NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA CHA MKOA WA MWANZA, JACKSON SONGORO NA KUSHOTO KWAKE NI MENEJA MAUZO WA TDL KANDA YA ZIWA MICHAEL MREMA

JEZI ITAKAYOTUMIKA KATIKA MECHI ZA  NYUMBANI

MECHI ITAKAYOTUMIKA KATIKA MECHI ZA UGENINI

WANAHABARI TULIOHUDHURIA

KAMPUNI ya Tanzania Distilers Limited (TBL) kupitia kinywaji chake cha Konyagi imetangaza kuidhamini timu ya Soka ya Mwanza United inayoshiriki michuano ya Ligi Daraja la kwanza inayotarajiwa kuanza kesho.
Akizungumza leo katika hafla ya kutangaza udhamini huo, meneja wa kinywaji hicho Martha Bangu alisema kwamba wameamua kuidhamini timu hiyo inayouwakilisha mkoa wa Mwanza ili kuipa nguvu ya kuweza kushiriki kikamilifu katika ligi hiyo.
Alisema kupitia udhamini huo ambao hata hivyo hakuwa wadhi kutamka kiasi cha gharama watakuwa wakiipatia timu hiyo fedha za nauli, malazi, chakula, posho za wachezaji pamoja na fedha nyingine kwa ajili ya uendeshaji wa timu.
Naye Mkurugenzi wa Mwanza United, Evarist Hagila aliishukuru kampuni hiyo kwa udhamini huo na kusema kuwa utawawezesha kushiriki kikamilifu katika ligi hiyo na hatimaye kuweza kupanda hadi ligi kuu mwakani.
Alisema watajitahidi mwaka jana walikosa pointi moja tu ili kuweza kupata nafasi ya kucheza katika Jackson Songoro tokana na timu hiyo kuuwakilisha mkoa katika ligi hiyo mwaka huu watahakikisha wanapanta pointi za kutosha zitakazowawesha kuwapa nafasi ya kushiriki ligi Kuu ya Vodacom mwakani.
Mwanza United itaanza ligi hiyo kesho kwa kukipiga na JKT Oljoro mjini Arusha, pia ipo kundi moja na timu za Rhino, Polisi Tabora, Polisi Morogoro na 94 Kj.

Comments