KID BWAY ARUHUSHIWA HOSPITALI

KID BWAY
MTANGAZAJI WA Redio Free Afrika na mmiliki wa studi ya Tetetemesha iliyopo jijini Mwanza, Sandu George Mpanda maarufu kama 'Kid Bway' aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza, ameruhusiwa leo mapema.
Habari kutoka kwa watu wa karibu wa mtangazaji huyo zinasema kwamba madaktari walimruhusu baada ya hali yake kutengemeaa lakini hata hivyo atakuwa akiendelea kumeza vidonge kwa muda wa mwezi mmoja huku akitakiwa kwenda hospitalini tena Oktoba 19 kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya afya yake.
Kid Bway alilazwa hiospitalini hapo kwa karibu wiki tatu baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na kupigwa na kitu kizito kichwani nyumbani kwake na kitendo hicho kilifanywa na mtu ambaye alikwenda na kujitambulisha kama msanii hivyo anataka kurekodi.
Kutokana na uvamizi huo, mtangazi huyo alikutwa akitutwa na majerha sehemu za kichwani huku damu zikimtoka masikioni na puani na ndipo alikimbizwa katika hospitali hiyo ambapo alipoteza fahamu kwa siku baada ya kufanyiwa tukio hilo la kinyama.
Kid Bway ni mmoja ya watayarisha=ji waliojipatia umaarufu jijini humo na Tanzania nzima kwa ujumla kutokana na jkazi anazozifanya kukubalika ambapo kwa sasa ndiye meneja wa msanii anayekuja kwa kasi Sajna, ambaye hivi karibuni aliachia albamu yake ya kwanza iitwayo 'Iveta'.
KILA LA HERI KAKA KATIKA KUJIUGUZA KWAKO NA MWENYEZI MUNGU ATAKUPONYA ZAIDI NA UENDELEE NA SHUGHULI ZAKO.

Comments