JAHAZI MODERN TAARAB WATAFANYA MAMBO MBAGALA KUU OKTOBA 15

WAKALI wa muziki wa taarab nchini kundi la Jahazi Modern ‘Wana Nakshi Nakshi’ chini ya Mzee Yusuf, oktoba 15 linatarajiwa kutoa burudani kwa wakazi wa Mbagala na maeneo jirani kupitia onyesho lililopewa jina la ‘Usiku wa My Valentine’, imefahamika.

Mratibu wa onyesho hilo Asha Said alisema litafanyika katika ukumbi mpya na wa kisasa wa Nawina Resort uliopo Mbagala Kuu.
Alisema onyesho hilo ni maalum kwa kuwapa raha mashabiki wa burudani na muziki wa taarabu kwa ujumla wanaoishi maeneo hayo na jirani ambao kwa muda mrefu hawajapata kupata uhondo toka kwa kundi hilo bora Tanzania kwa muziki huo.
Kundi hilo kwa sasa linatamba na albamu yake ya ‘My Valentine’ ambayo inaundwa na vibao kadhaa ambapo baadhi yake vinaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini, pia litapiga nyimbo zake zilizopo katika albamu za nyuma.
My Valentine ni albamu ya sita ya kundi hilo ambayo ilizunduliwa mwezi julai 30 mwaka huu inaundwa na vibao kama ‘My Valentine’ uliobeba jina la albamu, ‘Langu Rohoni’ , ‘Wema hazina kwa Mungu’, ‘Jalali Mungu Haikimbiliki’, Hundred Percent’ na ‘Mfa Maji’.

Comments