'GOMA LA MANZESE' WA TIP TOP CONNECTION HWANI WIKI IJAYO

                                               MENEJA WA TIPTOP CONNECTION, BABU TALE AKISALIMIANA NA RAIS          WA    TANZANIA, JAKAYA KIKWETE

VIDEO pamoja na singo ya pili ya kundi la muziki wa kizazi kipya Tip Top Connection ijulikanayo kama ‘Goma la Manzese’ inatarajiwa kusambazwa wiki ijayo katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni nchini, imefahamika.


Meneja wa kundi hilo lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam Babu Tale amesema leo  kwamba kazi ya kuihariri video hiyo iliyopigwa picha na Visual Lab imekamilika na sasa wapo katika mchakato wa kuandaa mipango ya kuiachia hewani ili kuwapa fursa mashabiki ya kupata burudani.

Tale aliongeza kuwa mara baada ya kuachia singo hiyo wataanza kujipanga kwa ajili ya kuachia albamu ya kundi hilo ‘Bado Tunapanda’ ambayo ilizinduliwa siku ya Idd Mosi huku tayari kibao kilichobeba jina la albamu kikiendelea kufanya vema katika chati za muziki.

Aidha, Tale alisema kundi lake linatarajkiwa kufanya ziara katika miji mbalimbali hapa nchini ziara ambayo ina lengo la kutangaza albamu hiyo iliyobebwa na nyimbo kumi kali, huku kazi ya kuitayarisha ikifanywa katika studio tofauti.

Wasanii wanaounda kundi hilo ni pamoja na Ahmed Ally ‘Madee’, Haridi Tunda ‘Tundaman’, Rushard Tunda ‘Richard’, Kassim Mganga ‘Cassim’ na Desso.

Comments