FLORIAN KAIJAGE ATIMULIWA TFF, KISA WIMBO WA TAIFA KUKATA WAKATI WA MECHI YA STARS NA MOROCCO

ALIYEKUWA OFISA HABARI WA TFF, FLORIAN KAIJAGE

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limemsimamisha Ofisa Habari wake, Florian Kaijage baada ya tukio la kutoimbwa nyimbo za Mataifa husika katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki kombe la Mataifa ya Afrika kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Morocco, mchezo uliochezwa Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tukio la kushindwa kuimbwa nyimbo za Taifa, lilitokea pindi rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, wageni kutoka Morocco na mataifa mengine, Watanzania waliojitokeza na nchi nyingine nyingi zilizoshuhudia mchezo huo.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga alisema baada ya kumsimamisha Ofisa huyo TFF wanaomba radhi kwa rais Kikwete, wapenzi na mashabiki waliojitokeza uwanjani, Watanzania kwa ujumla na wageni kutoka Morocco kwa tukio lile na kueleza kwamba tukio kama lile halitotokea kwa mara nyingine.
Tenga alisema ili kukwepa tukio kama hilo kuanzia sasa hata kama mitambo ya uwanjani ni mizima patakuwepo pia bendi za Polisi na jeshi la Wananchi (brass band) amam mitambo ya tahadhari kwa ajili ya nyimbo za taifa na matangazo mengine.
Aidha Tenga alisema tukio hilo haliishii kwa Kaijage na badala yake litahusisha waliopewa dhamana ambako watakaohusika watawajibishwa baada ya kuwasiliana na viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni kuhakikisha kuwa ucnhunguzi wa kina unafanyika kubaini kilichotokea.
“Tukio la kutopigwa kwa nyimbo za Taifa kama ilivyopangwa ilisababisha fedheha mbele ya rais Jakaya Mrisho Kikwete, halaiki iliyokuwepo uwanjani, wageni wa hapa nchini na dunia nzima, kwa sababu lingeweza kuzuilika kwa kutoa taarifa kama lilikuwa limeshindikana, kuliko fedheha hiyo,” alisema Tenga.
Awali kabla ya kutokea tukio hilo muda wa Kaijage kulitumikia Shirikisho hilo ulikuwa umemamilizika tangu Juni 30, baadaye TFF ilimuongezea muda wa kuliongoza Shirikisho hilo.
Tenga alisema baada ya kutokea matukio hayo anawajibika kuomba radhi kwa rais Jakaya Kikwete, wapenzi, Serikali ya Morocco na wananchi wake ambako atawasilisha barua kwa rais Kikwete kumuomba radhi sambamba na ubalozi wa Morocco na Serikali yake kwa tukio hilo.
Alisema pamoja na kusimamishwa kwa Kaijage, wiki ijayo TFF inatarajia kuanza mchakato wa kusaka Ofisa Habari atakayechukua nafasi hiyo sambamba na Katibu Mkuu inayokaimiwa na Sunday Kayuni.
Katika hatua nyingine Tenga alizungumzia kipigo cha Stars ilichokipata kutoka kwa Morocco, alitoa wito kwa Watanzania kutokata tamaa na badala yake ni kusaka jitihada zitakazofanikisha ushiriki wa kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2012.
Tenga alisema matumaini ya Stars kushiriki kombela Mataifa ya Afrika na badala yake ni kuongeza jitihada kuelekea mchezo kati ya Stars na Afrika ya Kati ambako kabla ya hapo Stars itashiriki kombe la Chalenji.
Kuhusu tukio la kusambazwa vipeperushi vilivyokuwa vikimtangaza rais Kikwete kwa aliyoyafanya katika medani ya soka hapa nchini ambako alisema TFF haina upande wa kisiasa na kusema jambo lile halihusiani na TFF.

Comments