BONANZA LA OTHMAN KAZI LAFANA VIWANJA VYA LEADRES LEO



BONANZA maalum la kuadhimisha miaka 14 ya kifo cha muasisi wa Taifa Mwalim JK Nyerere lililoandaliwa na mwamuzi wa soka Othman Kazi na kufanyika katika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam limefana baada ya timu zilizoshiriki michezo ya pete na soka kuonyesha ushindani wa hali ya juu.
Aidha bonanza hilo p[ia lilialika watoto toka kituo cha watoto yatima cha New Life ambapo walishiriki na wafanyakazi toka makampuni mbalimbali yaliyoshiriki katika bonanza hilo.
Makampuni hayo ni pamoja na Coca Cola, benki za CRDB, NMB, Baclays, Bibi Biskut, Toyota, Hazina, Tanzania,Albino United na mengineyo.

Comments